Uislamu na Mtindo wa Maisha mada kuu ikiwa ni kuhusu suala lal afya na siha. Miongoni mwa mambo muhimu katika mtindo wa maisha ni kutiliwa maanani masuala ya afya na siha. Hii ni kutokana na kwamba hapana shaka kuwa siha na afya vina taathira kubwa katika mtindo wa mtu wa maisha. Katika upande mwingine mtindo wa maisha wa mtu yeyete una nafasi muhimu katika afya na siha ya mwili wake. Katika maisha yake ya kila siku mwanadamu anahitaji mwili wenye afya na siha na suala hilo ndilo linalomwezesha kufanya kazi na shuguli zake nyingine za kimaada na kimaanawi. Uzima na siha ni miongoni mwa neema kubwa za Mwenyezi Mungu na aghlabu ya watu hutambua umuhimu wa neema hiyo baada ya kuondokewa nayo. Imam Swadiq (as) amesema: Afya na siha ni miongoni mwa neema zilizojificha, inapokuwapo husahauliwa, na inapoondoka ndipo inapokumbukwa." Vilevile babu yake, mtukufu Mtume Muhammad (saw) anasema: Wanadamu daima hukufuru neema mbili, neema ya afya na neema ya usalama."

Hapana shaka kuwa iwapo mwanadamu hatakuwa na siha na afya hawezi kufanya kazi yoyote yenye maana na wakati huo atahitajia watu wengine kufanya kazi zake za kila siku. Ni kwa sababu hiyo ndiyo maana pamoja na kusisitiza sana juu ya siha na uzima wa roho na fikra, Uislamu pia unatilia mkazo uzima, afya na siha ya mwili.

Hata hivyo tunapaswa kuelewa kuwa sisitizo la Uislamu juu ya afya na siha ya mwili halina maana ya kile kinachoonekana katika dunia ya sasa kwa maana ya kulea na kutunisha mwili na misuli. Kama tunavyojua, neema zote ambazo Mwenyezi Mungu amemtunuku mwanadamu ikiwemo ya afya na siha ni kwa ajili ya kuzitumia katika njia ya kufikia saada ya dunia na Akhera. Imam wa Wachamungu, Ali bin Abi Twalib (as) anasema: Zaka ya elimu ni kuisambaza, zaka ya urembo ni kujisitiri, zaka ya mwili ni jihadi na kufunga saumu na zaka ya afya na siha ni kufanya jitihada katika kumtii Mwenyezi Mungu.

Kwa kawaida mtu asiyekuwa na maradhi ya kimwili huitwa kuwa ni mzima na mwenye afya. Hata hivyo uzima, siha na afya vina maana pana zaidi. Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema kuwa uzima, siha na afya vina maana ya kudhamini mahitaji na burudani zote za kimwili, kiroho na kijamii na si kutokuwa na maradhi au nakisi ya kiungo cha mwili pekee. Kwa utaratibu huo mtu asiye na maradhi ya kimwili hawezi kutambuliwa kuwa ni mzima na mwenye siha bali mtu mwenye siha na afya kamili ni yule mwenye uzima na siha ya kiroho na kimwili kwa pamoja na mwenye utulivu katika upande wa masuala ya kijamii. Utafiti wa kisayansi unaonesha kuwa, chanzo cha matatizo mengi ya kimwili ni matatizo ya kiroho na kifikra. Kwa mfano msongo wa mawazo na matatizo ya kifikra vinaweza kuwa sababu ya maradhi ya utumbo. Hivyo basi, kwa kuwa matatizo mengi ya kifikra na kiroho ya mwanadamu yanatokana na mahusiano yake na wanadamu wenzake na vilevile matatizo ya kiutamaduni ya jamii, uzima na siha ya mwili vinafungamana kwa kiwango kikubwa na afya na siha ya fikra na mazingira ya kiutamaduni na ya kijamii katika jamii husika.

Afya kiistilahi ina maana ya harakati na hatua zote zinazochukuliwa kwa ajili ya kuboresha na kunyanyua juu afya na uwezo wa mtu au jamii ambayo ni pamoja na elimu na mbinu zinazosaidia kulinda afya na uzima wa mtu na jamii. Sasa hebu tutazame misingi na nguzo za mfumo wa afya na siha katika Uislamu.

Kwa kuwa afya na siha ni miongoni mwa mahitaji ya kimaumbile na yanayolinda na kudumisha kizazi cha mwanadamu, Uislamu umetayarisha mazingira mazuri ya kufikiwa malengo hayo kwa kuharamisha vitu vichafu, vyenye madhara na khabithi na kuhalalisha vilivyo safi, salama na mwendo wa wastani katika kitu. Sheria na kanuni za afya za Uislamu zimebuniwa na kuelezwa kwa njia nzuri na ya kuvutia ili ziweze kuoana na kuwiana na maumbile asili ya mwanadamu. Huwenda pia suala la kuwekwa kanuni za afya na siha katika mafundisho ya dini ya Uislamu ni kwa sababu ya Mwenyezi Mungu ameiweka hisi ya kupenda usafi na vitu visafi na salama na hisi ya kuchukia na kujiepusha na uchafu na vyenye madhara kwa mwili na roho ya mwanadamu katika maumbile ya asili ya mwanadamu. Aya ya 30 ya suratul Rum inasema: "Elekeza uso wako sawasawa kwenye dini ambayo ndilo umbile la Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu. Hapana mabadiliko katika maumbile ya Mwenyezi Mungu...."

Kwa mujibu wa aya hii, mafundisho na sheria za Uislamu zimetayarishwa kwa mujibu wa fitra na maumbile ya asili ya mwanadamu na maslahi yote ya kiumbue huyo yamezingatiwa katika mambo yote yaliyohalalishwa au kuharamishwa na sheria za dini hiyo. Imam Sadiq (as) anasema: Mwenyezi Mungu aliyeumba viumbe anajua ni vitu gani vyenye faida kwa miili yao na kwa msingi huo alivihalalisha na kuviruhusu na akaharamisha na kukataza vile vye madhara kwa miili yao."

Kwa kuwa masuala ya afya na siha yana umuhimu mkubwa sana, Mwenyezi Mungu Mtukufu aliamua kuyaweka baadhi ya masuala hayo katika taratibu za kiibada za Waislamu. Suala hili la kuwekwa masuala ya afya na siha katika mafundisho ya dini lina maana ya dhamana ya utekelezaji wake kutokana na umuhimu wake kwa mwanadamu. Kwani pale masuala hayo yanapowekwa katika safu ya mambo ya wajibu na ya lazima kutekelezwa, itakuwa muhali kwa Mwislamu anayeheshimu mafundisho ya dini kuyapuuza au kuyaacha.

Hivyo basi Mwislamu yeyote anayeelewa kwamba jambo lolote linalosababisha utulivu, afya na siha kwa Waislamu na wanadamu wenzake linamridhisha Mola wake Muumba, ataharakia kulinda usafi wa mazingira na kusaidia jitihada za kuimarisha afya ya umma. Mwislamu kama huyo hatakuwa radhi hata kidogo kumwaga au kutupa taka katika maeneo ya umma, kuchafua maji na mazingira, kuharibu misitu na vyanzo vya maji na kadhalika na daima huwa na mlinzi wa ndani ya nafsi anayemzuia kufanya mambo kama hayo.

Uislamu umehimiza sana juu ya afya na usafi na kuvitambua kuwa ni sehemu ya imani ya mja. Kwa hakika miongoni mwa sifa makhsusi za Uislamu ni kuwahamasisha wafuasi wake kulinda na kuchunga usafi na afya katika mambo yote ya maisha yao. Dini hiyo iliyaweka mambo ya usafi na afya katika taratibu za kiibada za dini hiyo na Mtume Muhammad (saw) amesema: Usafi ni katika imani. Vilevile amewahimiza Waislamu kuwa wasafi na kula vilivyosafi na salama kwa kusema: Chungeni usafi kadiri mnavyoweza kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu ameujenga Uislamu kwenye msingi wa usafi."

Hivyo basi mpenzi msikilizaji usafi na afya vimepewa nafasi maalumu katika Uislamu na wafuasi wa dini hiyo wanalazimika kuyatambua masuala hayo kuwa ni sehemu ya imani na itikadi za dini yao.

Mfumo wa afya na siha wa Uislamu umeweka ratiba kamili ya afya ya mtu binafsi na jamii katika pande zote za kimwili na kiroho. Mfumo huo una sheria za afya na siha ya mtu binafsi, familia, jamii, mazingira ya kazi, siha na afya inayohusiana na chakula na kadhalika. Kwa mfano tu aya ya 169 ya Suratu Maryam inawaamuru Waislamu kula vyakula halali na visafi na ile ya 24 ya Suratu Abasa inawataka wawe makini kuhusu vyakula wanavyochagua kwa ajili ya kula, uhalali wake na kadhalika. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, chakula kina mchango mkubwa katika uzima, siha na afya ya mwili na roho ya mwanadamu. Katika masuala hayo ya afya na uzima wa mwili na roho Mtume Muhammad (saw) anasema: "Sisi ni kaumu ya watu ambao hatuli chakula ila pale tunapohisi njaa, na tunapokula basi hatushibi na kujaza matumbo." Vilevile anasema katika hadithi nyingine kwamba: "Utumbo ni nyumba ya maradhi yote, na kujiepusha kula hadi kujaza tumbo ndio msingi wa dawa zote." Wasii na khalifa wake, Imam Ali bin Abi Twalib pia alimuusia mwanaye Imam Hassan (as) kwa kusema: Unataka nikufunze mambo manne yatakayokukinga na maradhi? Alisema ndiyo. Imam alisema: Usiketi kwenye meza ya chakula ila unapokuwa na njaa na usiondoke kwenye meza ya chakula ila ukiwa bado una hamu ya kula. Tafuna vyema chakula na nenda msalani kabla ya kulala. Utakapotekeleza mambo hayo yote basi kamwe hutahitaji dawa na tiba nyingine."      

>>>

Agmo Uislamu na Mtindo wa Maisha-27

Assalamu Alaykum wapenzi wasikilizaji na karibuni kuwa nasi tena katika sehemu nyingine ya kipindi chenu cha Uislamu na Mtindo wa Maisha. Katika kipindi cha wiki iliyopita tulianza kuzungumzia suala la afya na usafi katika mtindo wa maisha wa Kiislamu. Kipindi chetu cha leo kitaendeleza maudhui hiyo. Karibuni.

  

Kama bado mnakumbuka tulisema katika kipindi cha wiki iliyopita kwamba afya ina maana ya majmui ya shughuli na harakati za kuboresha na kuinua juu kiwago cha siha na uwezo wa mtu na jamii kwa ujumla. Hatua kama hizo ni pamoja na elimu na mbinu zinazosaidia kuboresha na kuimarisha afya na siha ya mtu na jamii.

Hapana shaka kuwa itikadi za kidini za kila jamii huwa na mchango mkubwa katika uzima na siha ya watu wa jamii hiyo. Katika upande huo dini ya Uislamu imeipa umuhimu mkubwa roho na mwili wa mwanadamu kwa kadiri kwamba, katika kuhimiza na kuwahamasisha wafuasi wake kuhusu suala la kuchunga na kulinda afya zao, imebainisha na kusisitiza sana juu ya athari zake za kimaada na kiroho na taathira zake za kiduni na ulimwengu wa Akhera. Huwenda pia tunaweza kusema kuwa, uhamasisho mkubwa zaidi wa Uislamu kwa masuala ya kiafya ni kueleza taathira zake katika kupata radhi na mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Maneo kama "tayyibat" kwa maana ya vitu visafi na neno "twahara" kwa maana ya usafi vimekaririwa mara kadhaa katika Qur'ani Tukufu, suala ambalo linaonesha umuhimu mkubwa wa afya na siha ya mwili na nafsi katika mafundisho ya Uislamu. Kwa kuwa mwili ndiyo merikebu na chombo kinachobeba roho na kulinda afya na siha yake kuna taathira kubwa sana katika roho ya mwanadamu, mafundisho mengi ya Uislamu yaliyoelezwa katika sheria za fiqhi yamelizingatia na kulipa umuhimu suala la afya, uzima na siha.

Miongoni mwa masuala ambayo yana mchango mkubwa katika afya na siha ya mwanadamu ni mtindo wa maisha na na taratibu na desturi za kula na kunywa. Suala hilo pia limepewa mazingatio katika mafundisho ya Qur'ani Tukufu ambayo imetilia mkazo suala la kuchunga mwenendo wa wastani katika kula na kunywa. Mwenyezi Mungu SW anasema katika aya ya 31 ya Suratul Aaraf kwamba: Kuleni na kunyweni wala msifanye ufujaji, hakika Yeye (Mwenyezi Mungu) hawapendi wafanyao ufujaji.

Maagizo hayo ya Qur'ani ni kanuni kuu ya afya na siha ambayo ina mchango mkubwa katika afya na uzima. Utafiti uliofanywa na wataalamu wa afya umebaini kuwa, chanzo cha maradhi mengi ya mwanadamu ni chakula ziada anachokula kiumbe huyo ambacho kalori zake hubakia mwilini bila ya kutumika. Nishati hiyo inayobaki mwilini huwa mzigo mkubwa kwa moyo na viungo vingine vya mwili na huwa chanzo na sababu ya maradhi mengine. Sababu kuu ya kalori hizo ni chakula ziada au kwa maneno mengine kula chakula kingi. Kula chakula kingi huwa sababu ya maradhi ya kisukari, ukakamavu wa mishipa, mafuta mengi kwenye damu, matatizo ya ini, kunenepa kupita kiasi na aina mbalimbali za ugonjwa wa kiharusi.

Mafundisho ya Uislamu kuhusu jinsi ya kula na kunywa yanadhamini uzima, siha na afya ya mwili na roho ya mwanadamu. Mtume wetu Muhammad (saw) anasema: "Jiepusheni kula sana kwani kufanya hivyo kunaufanya moyo kuwa na ukatili, kunavitia viungo uzembe wa kumtii Mwenyezi Mungu na kuyafanya masikio yasisikie hekima na mawaidha." Imam Ali bin Abi Twalib (as) pia amesema: Mtu anayetosheka kwa kula chakula kichache huwa na siha zaidi na fikra bora." Imam Jaafar Swadiq (as) pia amesema: "Mtu anayetaka kuwa na siha na mwili wenye nishati, apunguze chakula chake cha usiku."

Imenukuliwa katika kitabu cha tafsiri ya Qur'ani cha Majmaul Bayan kwamba, mtawala Haroun Rashiid alikuwa na tabibu Mkristo ambaye umahiri wake mkubwa katika masuala ya tiba ulikuwa maarufu sana baina ya watu. Siku moja tabibu huyo alimwambia msomi wa Kiislamu kwamba: Sipati chochote kuhusu masuala ya tiba katika kitabu chenu cha mbinguni yaani Qur'ani, ilhali elimu zenye faida ni mbili: Elimu ya dini na elimu ya miili. Msomi Mwislamu alijibu kwa kusema: Mwenyezi Mungu ameweka kanuni zote za tiba katika nusu ya aya ya kitabu chake, Qur'ani, na Mtume wake pia ameweka kanuni hizo katika hadithi inayosema: "Utumbo ni nyumba ya maradhi yote na kupunguza kula ndiyo kinara wa tiba zote."  Baada ya kusikia maneno hayo Tabibu Mkristo alisema: "Qur'ani yenu na Mtume wenu hawakumbakishia Jalinos kanuni yoyote mpya ya tiba." Jalinos huyu anayetajwa na tabibu Mkristo alikuwa gijwi la tiba la Kigiriki. 

                 >>>>>>

Suala la kuchunga adabu na desturi nzuri za kula na kunywa linaonekana kwa wingi katika sira na mwenendo wa Mtume Muhammad (saw) na Ahlibaiti zake watoharifu. Imepokewa kuwa Imam Hassan bin Ali (as) alisema kuhusu baadhi ya adabu na kanuni za kula kwamba: Tonge la chakula linapaswa kuwa ndogo, chakula kinapaswa kutafunywa barabara na si vizuri kuwatazama usoni watu wengine wanaukula. Vilevile Imam Swaqid (as) anasema: "Mtu anayeosha mikono yake kabla na baada ya kula chakula huwa amekitia baraka chala chake na kujikinga na maradhi ya mwili."

Kuhusu adabu na sira ya Mtume (saw) wakati wa kula, imepokewa kwamba mtukufu huyo alikuwa akiwakataza watu kupuliza kwenye chakula na kinywaji na amesema katika hadithi nyingine kwamba: Msiache vyombo vyenu bila ya kufunikwa.

Suala jingine linalosaidia afya na siha ya mtu ni usafi na kuwa nadhifu. Usafi umepewa umuhimu mkubwa sana katika Uislamu kwa kadiri kwamba, Mtume (saw) ameutaja kuwa ni alama na dalili ya Imani ya mja.  Usafi na unadhifu umesisitizwa sana katika Uislamu kiasi kwamba wanazuoni wa fiqhi wa Kiislamu wametenga mlango maalumu unaozungumzia usafi mwanzoni mwa vitabu vyao vya fiqhi na sheria za Kiislamu. Suala hili linaonesha kwamba amali nyingi za mwanadamu haziwezi kutimia na kukubalika bila ya kuzingatiwa usafi. Mtume Muhammad (saw) amesisitiza sana juu ya suala la usafi kwa kutumia maneno mbalimbali. Anasema katika hadithi moja kwamba: "Jisafisheni sana ili muzidishiwe umri na Mwenyezi Mungu SW." Vilevile anasema: "Uislamu ni nadhifu, basi kuweni wasafi na nadhifu, kwa sababu hataingia peponi isipokuwa mtu nadhifu."

Vilevile baadhi ya hadithi zinasisitiza kuwa kuchunga kanuni za usafi kuna matunda mbalimbali na miongoni mwa matunda hayo ni kuzidishiwa umri, kuwa na afya na siha, kuwa na uzima wa mwili na roho, kupata radhi na kupendwa na Mwenyezi Mungu, kukamilika imani ya mtu, kupata baraka, kuondokewa na umaskini na kadhalika.

Imepokewa kwamba Mtume (saw) alikuwa kigezo cha usafi na suala hilo limesisitizwa sana hata ndani ya Qur'ani Tukufu. Aya ya 4 ya Suratul Muddathir inasema: Na nguo zako zitwahirishe. Vilevile Mtume (saw) daima alikuwa akiwausia maswahaba zake kuwa wasafi na maridadi na amesema: Safisheni mavazi yenu, punguzeni nywele zenu na kuweni maridadi na wasafi. Mfasiri mkubwa wa Qur'ani wa zama hizi Allamah Muhammad Hussein Tabatabai amesema: Nguo nyingi za Mtume Muhammad (saw) zilikuwa za rangi nyeupe na mtukufu huyo daima alikuwa akisema: "Wavikeni watu hai mavazi meupe na wazikeni waliokufa kwa mavazi meupe." Kutokana na weupe wake, mavazi hayo huonesha uchafu haraka na wazi zaidi na kumlazimisha aliyeyavaa kuyavua na kuyasafisha mapema.

Wanahistoria wanasema Mtume Muhammad (saw) alikuwa akionekana msafi kupita watu wote na aliwahimiza mno Waislamu kujipaka manukato, kuchana nywele na kupiga mswaki na yeye mwenyewe alikuwa mstari wa mbele katika mambo hayo. Hii leo wapenzi wasikiliza, imethibitika kuwa usafi wa mdomo na meno ni miongoni mwa mambo muhimu katika kulinda siha na afya ya wanadamu. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, vijidudu maradhi wengi huingia mwilini kupitia njia ya mdomo. Mtume (saw) alilipa umuhimu mkubwa suala hilo na alikuwa akiwaambia masahaba zake kwamba: "Midomo yenu ni njia na kuvuko cha Qur'ani, hivyo isafisheni kwa kupiga mswaki." 

  >>>>

Wapenzi wasikilizaji kipindi chetu cha leo kimeishia hapa. Ni matarajio yangu kuwa mnenufaika na yale tuliyokuandalieni. Asanteni kwa kututegea sikio na kwaherini....

Agmo Uislamu na Mtindo wa Maisha-28

Hamjhambo wasikilizaji wapenxzi na karibuni kuwa nami tena katikja sehemu nyingine ya kipindi chenu cha kila wiki cha Uislamu na Mtindo wa Maisha. Lipindi chetu cha leo kitaendelea kujadili umuhimu wa afya na siha katika mtindo wa maisha wa Kiislamu.

Kuwa na afya na siha ni miongoni wma haki za mtu binafsi na jamii. Uchunguzi wa ndani ya aya za Qur'ani Tukufu na vitabu vya wanazuoni wa Kiislamu unaonesha kuwa dini hii tukufu ya Mwenyezi Mungu umelipa umuhimu mkubwa suala la afya, uzima na siha ya mtu na jamii. Tunaweza kusema kuwa hakuna dini au mfumo wowote mwingine wa kifikra na kujiamii uliohimiza mno suala la afya na siha kama Uislamu. Dini hii imebainisha masuala mengi ya afya katika kalibu ya sheria za fiqhi. Kwa mfano dini hiyo imeharamisha kula vitu kama damu, mnyama ya mzoga, nyama ya wanyama walioharamishwa, udongo, pombe na vileo vinavyoondoa akili ya mwanadamu na kuhatarisha afya yake na kadhalika.

Katika upande mwingine mafundisho ya Uislamu yameyaweka masuala mengi ya afya yenye nafasi muhimu sana katika afya na siha ya mwanadmu katika sura ya wajibu au mustahabu na suna. Kwa mfano miongoni mwqa mambo yanayoambatana na ibada ya Swala ni twahara ya mwili na mavazi anayetaka kuswali na kutia udhu ambako kumetambuliwa kuwa ni wajibu kwa ajili ya kutekeleza ibada hiyo. uchunguzi wa kina katika sheria za Kiislamu unaweka wazi ukweli kwamba kila moja kati ya sheria hizo ina hekima na falsafa maalumu ambayo huwenda wengi wengi wahazujui. Suala pekee tunalolitambua ni kwamba katika falsafa ya sheria hizo kuna maslahi yanayohimizwa au madhara yanayokatazwa kuhusu mwili au roho ya mwanadamu. Kila kitu kinachokuwa na faid na maslahi kwa mwili na roho ya mtu au siha na uzima wa jamii kimefanywa halali au wajibu na kile chenye madhara na hasara kwa mtu au jamii kumeharamishwa.

Hapa tunapaswa kutaja nukta hii muhimu kwamba, katika Uislamu maslahi yanatangulizwa na kupewa kipaumbele zaidi kuliko manufaa kwani yuymkini jambo likawa na manufaa kwa mwanadamu lakini kwa ujumla lisiwe na maslahi kwake yeye au jamii.

Vilevile kuna kanuni inayokataza madhara na kuwasababishia madhara watu wengine, kuchafua mazingiraya maisha ya wanadamu, na kuwalazimisha watu kuchunga kanuni za afya ya mtu binafsi na jamii. Kwa mfano tu mwenyezi mungu SW amewaamuru Waislamu kuzika maiti zao kwa ajili ya kulinda uzima, afya na mazingira.

Kama tulivyotangulia kusema katika vipindi vilivyopita, suala la afya na misingi ya siha limehimizwa sana katika Uislamu wka kadiri kwamba Mtume (saw) alilitaja kuwa ni katika alama za imani ya mja. Hii ni kwa sababu katika Uislamu kila amali inayofanyika kwa nia ya kutekeleza wajibu na amri ya Allah na kuwahudumia watu na jamii inatambuliwa kuwa ni ibada.

Kuwa na sifa ya mwili na roho ni katika mambo yanayafanya maisha jkuwa yenye utulivu na kutayarisha uwanja mzuri wa kuwa mja mwema wa M, Mungu. Wkani ili kuweza kuwa mja mwema wa Allah, mwanadamu anahitaji kuwa na mwili mzima na wenye afya na sifa. Kwa msingi huo mafndisho ya Uislamu yamewajibisha suala la kulinda afya ya mwili na nafsi na hayawaruhusu wafuasi wa dini hiyo kuudhuru mwili na nafsi hata wakatri wa kipindi cha mashaka na misiba mikubwa. Baadhi ya hadithi zinasisitiza kuwa mwili na viungo vyake ni amana ya Mwenyezi Mungu kwa wanadamu na kwamba kulinda na kuchunga amani ni katika sifa muhimu za waumini wa kweli. Mtume (saw) amesema: Sikio, jicho, ulimi na moyo ni amana, na kila mtu asiyelinda amana hana imani."

Mfumo wa mwili wa mwili wa mwanadamu umetayarishwa kwa njia ambayo iwapo misingi na kanuni zote za usafi, afya na siha za mtu binafsi na jamii zitalindwa na kuchungwa basi asilimia ya maradhi yanayompata mwanadamu itapungua wka kiwango kikubwa na huwenda kutoweka kabisa. Hata hivyo mtindo usio sahihi wa maisha ya mwanadamu unamuweka kiumbe huyo katika hatari ya kukumbwa na matatizo na maradhi ya aina mbalimbali.

Wapenzi wasikilizaji katika kipindi kipichopita tulizungumzia baadhi ya hadithi za Mtume na Ahlibaiti zake zinazobainisha adabuna taratibu kula na kunywa kwa njia sahihi kama hadithi ya Mtume iliyosema: Tumbo ndiyo nyumba ya maradhi yote na kujiepusha kula sana ni dawa la kila maradhi. Hivyo basi kuleni vyakula vinavyowiana na miili yenu".

Suala jingine linalosaidia katika uzima na afya ya mtu ni kupumzisha viungo vya mwili ambavyo ni muhimu kuwa na uadilifu na mwenendo wa wastani katika kuvitumia. Imam Ali bin Abi Twalib amesema: "Kuushinikiza moyo kunazuia fahamu, kwa sababu kila kiungo cha mwili kinahitaji kupumzika." Vilevile Imam Swadiq (as) amesema Mtu anayefanyakazi usiku na kitopumzisha mwili kwa sababu kukosa kulala (hadi akapatwa na madhara)basi kazi yake hiyo ni haramu japo itamuingizia mali ya halali."

Miongoni mwa nguzo muhimu za kudhamini uzima wa mwili na froho ya mwanadamu ni kuwa na moyo wa kuridhika na kutosheka maishani na kujiepusha na tamaa na pupa.