
Je, ni nini Qur an?
Qur an ni neno la kiarabu ambalo, katika maumbile limetokana na neno jingine la Kiarabu: ? Qara?a?, ambalo maana yake kwa mujibu wa wanavuoni wa fani za lugha ni: 1. Kusoma, na 2. Kuweka vitu pamoja.Hata hivyo, katika sheria ya Kiislamu neno hili linamaanisha kuwa ni maneno maalum ya Mwenyezi Mungu aliyoteremshiwa Mtume Muhammad SAW kupitia kwa Malaika Jibril a.s
Jibril a.s ni Malaika ambaye kazi yake kubwa ni kushusha Wahyi kutoka mbinguni kwenda kwa Mitume.
Lengo kuu la kushushwa maneno haya maalum ni moja tu, nalo ni kumuongoza binadamu katika kufikia uongofu ambao Mwenyezi Mungu mwenyewe ametaka binadamu aupate.
Qur'an inalithibitisha hili:
( Al- Baqarah: 185 )
Ni mwezi wa Ramadhani ambao, imeteremshwa hii Qur'ani ili iwe mwongozo kwa watu na hoja zilizo wazi za Mwongozo na ufafanuzi??????
Pia katika Sura ya pili , Aya ya kwanza tunasoma:
? Hicho ( Qur ani )ni kitabu ambacho hakina shaka ndani yake: Ni muongozo kwa wanaomcha Mwenyezi Mungu.?
Pamoja na kuwa Qur'ani ni mwongozo wa Allah kwa binadamu, pia ndani mwake mna maonyo na mazingatio kwa binadamu juu ya matendo yake hapa ulimwenguni, ili huyo binadamu asije akapoteza lengo la kuumbwa kwake na kuletwa kwake ulimwenguni.
Tunasoma:
( Sura ya 25, Aya ya 1 ).
? Ametukuka yule ambaye ameiteremsha Qur ani kwa mja wake ( Muhammad )ili iwe muonyaji kwa walimwengu ?.
Aya za Qur ani hazikuacha kumuasa binadamu asije akalisahau lengo la kuumbwa kwake na kuletwa kwake hapa duniani, kwani kujisahau kutambakisha kwenye hasara na majuto.
1- Naapa kwa zama( zako ewe Nabii Muhammad ).
2- Kwamba binadamu wamo katika hasara.
3- Ila wale ambao wameamini na kutenda matendo mema.
4- Na wakausiana Haki na wakausiana kuwa na Subra ?
Qur ani ni kitabu kilichotosheleza haja zote za binadamu katika maisha yake, na ni kitabu ambacho daima kimeutangulia wakati. Mwenye kukisoma, akayafahamu yaliyomo na kisha akayazingatia na kuyatumia maishani, anakuwa mtu bora kabisa hapa ulimwenguni, kwa sababu, hiyo ndiyo hasa kazi ya Qur ani, kuja kumkomboa mja dhidi ya vikwazo mbali mbali vinavyomkabili maishani, na kwa ajili hiyo, Qur ani haikubakisha kitu. Na ndiyo maana ALLAH mwenyewe akathibitisha kwamba ndani ya Kitabu hiki hamna shaka, bali mwongozo kwa wenye kukizingatia.
WAISLAMU TUSOME QURANI
TUKUFU TUFAHAMU TUTEKELEZE KWA VITENDO TUFIKIE LENGO ALILO KUSUDIA MOLA
WETU MTUKUFU TUPATE RAHA ZA DUNIANI NA AKHERA AMINA.
.